Genesis 33:1-6

Yakobo Akutana Na Esau

1Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. 2Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yusufu wakaja nyuma. 3Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake.

4Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. 5Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?”

Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”

6Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu.
Copyright information for SwhKC